Monday, 2 May 2016

MH. ELIBARIKI KINGU AFANIKIWA KUPATA AMBULENSI MBILI KWA AJILI YA JIMBO LAKE "SINGIDA MAGHARIBI".

Moja ya Gari la Kubea Wagonjwa, baada ya miezi miwili zitawasili Tanzania tiyari kwa kukabidhiwa Wananchi  wa Jimbo la Singinda Magharibi.
Mbunge wa Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu amefanikiwa kupata Ambulances mbili kwa ajili ya Jimbo lake Singida Magharibi, kutoka Africa Kusini Johanesburg.
Aliendelea kusema, Baada ya miezi miwili zitakabidhiwa kwa wananchi wake  anao wapenda sana.
Mwisho, alimaliza kwa kumshukuru aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. "Asante sana Mwanadiplomasia Benard Membe kwa kunipa mtu makini huko Johanesburg kunisaidia kupata Van hizi. Mungu akubariki kwa uzalendo wako mzee wangu.

Watu wangu ninawapenda tumejinyima wote kwa ustawi wa nchi yetu".

No comments:

Post a Comment