Saturday, 8 December 2018

SALAMU ZA RAIS MAGUFULI KUELEKEA SHEREHE ZA UHURU DESEMBA 9, 2018




*Atoa msamaha kwa wafungwa 4400, awapongeza awamu zote 
zilizopita
*Asisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana kujenga uchumi wa nchi 
yetu

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

RAIS wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk.John Magufuli amewatakia Watanzania wote nchini kutafakari tulikotoka, tulipo na tunakokwenda huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kufanya kazi ili kujenga uchumi imara hasa kwa kuzingatia kwa sasa tupo kwenye vita ya kiuchumi ambayo lazima wote tushirikiane kuishinda.

Ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati anatoa salamu za kuwatakia kila laheri Watanzania katika kuelekea kuadhimisha miaka 57 ya Uhuru wa Tanganyika Desemba 9, 2018 ambapo itakuwa Jumapili ya wiki hii na kufafanua siku hiyo itakuwa ni ya mapumziko, ambayo itumike kutafakari tulikotoka na tunakokwenda.

"Kila laheri Watanzania katika kusherehekea miaka 57 ya Uhuru wa Tanganyika.Kama ambavyo mnafahamu tayari fedha Sh.bilioni moja 
zilitengwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo lakini nimeshatoa maelekezo fedha hizo zitumike kujenga Hospitali Dodoma ambayo itaitwa Hospitali ya Uhuru,"amesema Rais Dk.Magufuli na kufafanua kwa kuwa Serikali inahamia Dodoma kuna umuhimu wa kujengwa kwa hospitali nyingine ili ziwepo mbili,"amesema.

Amesema kuwa tayari sehemu ya watumishi wa Serikali wapo Dodoma na amebaki yeye tu ambaye naye anajiandaa kuondoka siku za hivi karibuni na hivyo ndio maana ni muhimu kujengwa kwa hospitali ya pili ili isaidiane na Hospitali ya Mkapa.

Pia Dk.Magufuli amefafanua katika kutafakari siku hiyo ni vema ikakumbukwa kuwa baada ya kupata uhuru wa nchi yetu , sasa ni kuendelea na harakati za kujenga uchumi."Uhuru ambao tumeupata Desemba 9 mwaka 1961 ulikuwa ni mwanzo tu wa kutafuta Uhuru mwingine, uhuru wa kiuchumi ambao ni mgumu zaidi kuliko ule wa 
mwanzo."

Ametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa Serikali za Awamu zote kutokana na kutokana na mafanikio makubwa ambayo yamepatikana kwenye maendeleo ya nchi yetu kwani kuna mambo mengi yamefanyika kuanzia mwaka 1961.Pia amesema bado kuna safari ya kuendelea kujenga uchumi ikiwa pamoja na kuijenga Tanzania ya watu waliolimika, Tanzania ambayo itakuwa na huduma bora, Tanzania ambayo huduma za afya zimeboresha na Tanzania ambayo itajali makundi yote.

Pia amesema juhudi zinazoendelea za kujenga uchumi zimeifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tano ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi huku akielezea ndani ya miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano mitaji yenye thamani ya Sh.trilioni 30 ambazo zimeingia nchini na kuwekezwa kwenye maeneo mbalimbali.

Kuhusu vita dhidi ya rushwa amesema kumefanya jitihada kubwa za kukomesha rushwa nchini kwetu ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania kuendelea kuiunga mkono Serikali na kwamba 
kama ambavyo amesema .

No comments:

Post a Comment