Wednesday, 7 June 2017

MBUNGE COSATO CHUMI ATOA MSAADA WA AMBULANCE NYINGINE JIMBONI KWAKE


MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi akizungumza na wananchi wa Igohole wakati kukadhi gari la kubebea wagonjwa ambalo amepewa na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 
MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi sambamba na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mafinga Charles Makoga wakikata utepe wa gari la kubebea wangonjwa la kituocha afya cha Igohole
hawa ni baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa kupokea msaada wa gari hilo la kubebea wagonjwa lilotelewa na mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwa kushirikiana na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 


Na Fredy Mgunda,Mafinga

MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwa kushirikiana na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya kituo cha afya cha Igohole ya wilayani Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake hilo.

Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser lilikabidhiwa kwa uongozi wa halmashauri ya mji wa Mafinga inayosimamia uendeshaji wa kituo hicho katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Igohole, mjini Mafinga.

Akikabidhi msaada huo Chumi alisema; “napenda ifahamike kwamba gari hilo limenunuliwa na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Uadilifu na uaminifu kwa serilikali ndio umetufanya tushirikiane vyema katika mambo mengi kwa faida ya wananchi wa jimbo langu la Mafinga.”

Alisema gari hilo la wagonjwa ni rafiki kwa wagonjwa na wajawazito kwa kuwa lina vifaa tiba vinavyoweza kutumika kutolea huduma wakati wakipelekwa hospitalini.

Baada ya kukabidhi gari hilo, Chumi ambaye ni mbunge wa kwanza wa jimbo hilo jipya, mkoani Iringa alikumbusha vipaumbele vyake kwa wapiga kura wake kuwa ni kuhakikisha jimbo la mafinga mjini linapata huduma bora ya maji, elimu, afya na miundombinu ya barabara.

Akishukuru kwa msaada huo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Dk Innocent Mhagama alisema kabla ya msaada huo, kituo hicho cha afya kilikuwa hakina gari hata moja la kubeba wagonjwa.

“Pamoja na kuhudumia hospitali hiyo ya wilaya, kurikuwa na magari mawaili tu ambayo yalikuwakihudumia vituo vingine 18 vya kutolea huduma katika wilaya hiyo hivyo,” alisema Mhagama.

Alisema kupatikana kwa gari hilo jipya kutasaidia kuboresha huduma hiyo kwa kuokoa maisha ya wagonjwa na maisha ya mama na mtoto ambayo ni kipaumbele katika utoaji wa huduma za afya.

Akizungumzia huduma ya mama na mtoto katika hospitali hiyo ya wilaya, Dk Mhagama alisema kwa wastani wajawazito 500 wanajifunga kila mwezi hospitalini hapo.

“Kati yao wajawazito zaidi ya 100 huwa wanapata huduma za dharula huku wastani wa wajawazito 10 wakipatiwa huduma za rufaa,” alisema dr Mhagama.

Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Charles Makoga alisema halmashauri yake kwa kushirikiana na mbunge huyo itahakikisha inatekeleza ahadi mbalimbali zilizotolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk John Magufuli, mbunge na madiwani ili kuboresha huduma kwa watu wake.

No comments:

Post a Comment