Saturday, 8 December 2018

NAIBU WAZIRI MHE. KANYASU AENDESHA HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

1
  1. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ( wa pili kushoto)  akizungumza mara baada ya ibada iliyofanyika katika ya Kanisa la Wasabato la Geita kati wakati ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita
2
  1. Baadhi ya waumini ibada wa Kanisa la Wasabato la Geita kati wakifuatilia ibada kabla  ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.
3
  1. Mchungaji na  Mwenyekiti wa South Nyanza Conference, Sadoki Butoke akitoa mahubiri kwa  waumini waliojumuika katika ibada ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.
4
  1. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya watendaji wa mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa  Kanisa la Wasabato la Geita wakisikiliza mahubiri kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.
5(1)5(2)
  1. Baadhi ya wanakwaya wakiimba wakati wa mahubiri kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo  afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.
6
  1. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akivishwa skafu na vijana wanafunzi wa Skauti kanisa la Wasabato la Geita Kati kabla  ya Naibu Waziri huyo kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.
7
  1. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja  na kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita mara baada ya kusomewa taarifa ya hali ya uhifadhi wa misitu na wanyamapori kabala ya kushirikia harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Afya.
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)
……………………..
LUSUNGU HELELA-GEITA
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu  amesali katika Kanisa la Wasabato la Geita Kati  mkoani Geita ambako ameendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Afya.
Lengo la kuendesha harambee hiyo  ni kwa ajili ya kuchangisha pesa zitakazotumika katika ujenzi wa  Kituo  cha Afya cha Kanisa la Wasabato kinachotarajiwa kujengwa  katika  kata ya Bombambili  eneo la Magogo kitakachosaidia kuihudumia jamii.
Katika harambee hiyo Naibu Waziri Mhe. Kanyasu  aliambatana na wadau wake ambapo kwa pamoja waliweza kukabidhi   Sh15 milioni  zikiwa ni fedha taslimu kama mchango wao.
 Katika harambee hiyo, ahadi mbali mbali zimeweza  kutolewa  ikiwemo matofali, saruji  pamoja na malori  ya mchanga na mawe.
Sambamba na hilo, Mhe. Kanyasu  ameupongeza uongozi wa kanisa hilo kwa kuwa na mpango huo wa  kuisaidia serikali katika kutoa huduma kwa jamii ambayo kimsingi ni kazi ya Serikali,
”Suala la kujenga vituo vya afya ni jukumu la serikali lakini ninyi mmeamua kuisaidia serikali nawapongezeni sana na msisite kunishirikisha kwa lolote.
Aidha, Mhe. Kanyasu amewataka waumini  wa Kanisa hilo kuendelea kujitolea kukamilisha hatua  za ujenzi wa kituo hicho cha Afya
Kwa upande wake Mchungaji na  Mwenyekiti wa South Nyanza Conference, Sadoki Butoke amesema kituo hicho cha Afya mara baada ya kukamilikwa kwake kitatumika kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na sio kwa ajili ya kupata kitu
Ameongeza kuwa kituo hicho kitawasaidia kitasaidia kuijenga jamii  kiroho na kimwili na ili kukamilika kwake jumla ya sh 150 milioni zinahitajika.

No comments:

Post a Comment