Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde, amezindua rasmi Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma. Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road, Dodoma kwa kujumuisha wasanii wa ndani na nje ya Dodoma. Ofisi hizo na studio Zitatumiwa na Wasanii wote kupitia umoja wao na Vilabu vya wasanii.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge Mavunde amewataka wasanii wa Dodoma kuwa na UPENDO, MSHIKAMANO na UMOJA ili kuweza kufikia mafanikio na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanafika mafanikio ya juu katika sanaa.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh. Patrobas Katambi amempongeza Mbunge Mavunde kwa namna anavyowatumikia wanaDODOMA na kuahidi kushirikiana nae kuwasaidia Vijana wasanii ili wapige hatua zaidi katika mafanikio yao kwenye sanaa.
No comments:
Post a Comment