WATU wanne wanahisia kufariki dunia huku 12 wakiwa wamejeruhiwa vibaya, katika ajali iliyoyahusisha magari manne, mawili yakiwa katika msafara wa Kamati ya Bunge Utawala na TAMISEMI maeneo ya Kerege, Bagamoyo Pwani, anaandika Mwandishi Wetu.
Ajari hiyo iliyohusisha lori la mchanga, gari dogo yaliyokuwa yanatokea Bagamoyo kuja Dar es Salaam, na magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara wa Kamati hiyo, yaliyokuwa yanaenda Bagamoyo kwa shughuli zake za kibunge.
Magari yaliyokuwa katika msafara wa kamati hiyo, ni gari la Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na gari la Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo ambayo yaligongwa na lori hilo la mchanga na kusababisha vifo vya watu hao na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Ajali hiyo ilitokea baada ya gari dogo lililokuwa linatokea Bagamoyo kupunguza mwendo ghafla na kusababishwa lori lililokuwa nyuma yake kuligonga na kuhama upande wa pili na kuyagonga magari mawili yaliyokuwa katika msafara wa kamati ya Bunge.
Taarifa zaidi zitawajia hivi punde baada ya kupata taarifa kamili (Taarifa ya awali inaeleza hivyo sijawa na uhakika nayo moja kwa moja)
Sehemu ya Magari yaliyohusika kwenye ajali hiyo.
Hivi ndivyo ionekanavyo moja ya gari lililohusika kwenye ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment