Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesema ili fursa za ajira ziweze kuongezeka katika nchi za Afrika Mashariki na Kati, inapaswa kuondoa urasimu rushwa.
Hassan aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa mifuko ya jamii kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Ecassa) wa kujadili masuala mbalimbali, ikiwamo uboreshaji wa mifuko hiyo.
Alisema takwimu za ajira zinaweza kuongezekana kama upunguzwa urasimu pamoja na kuondokana na rushwa, kwani takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka mitano huajiriwa watu 1,000,000.
Alisema mambo hayo yakiondolewa kuna uwezekano mkubwa wa ajira kuongeza na hata uchumi kupanda katika nchi za Afrika Mashariki na kati.
No comments:
Post a Comment